Wanafunzi 7 hupata mimba kwa mwezi
.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Agnes Hokororo hadi kufikia Juni mwaka huu jumla ya wanafunzi 42 wa shule za msingi na sekondari wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito.
Takwimu hizo zimetajwa ni kwa kipindi hadi kufikia shule hizo zinafungwa mwezi mmoja uliopita ambapo mipango imewekwa kufanyiwa tena kwa vipimo kwa wanafunzi wote wa kike mara baada ya kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari Julai 3 mwaka huu
.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa huo, Anna Mghwira, mkuu wa wilaya hiyo, Hokororo amesema, “Itakumbukwa kwa kipindi cha mwaka jana jumla ya wanafunzi 63 walikatishwa masomo, juhudi zinaendelea kukabiliana na changamoto hii”.
Alisema pamoja na mimba za utotoni lakini pia katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu kumeripotiwa matukio 25 ya ubakaji na nane ya ulawiti, jambo ambalo linaashiria wananchi kukiuka utii wa sheria
No comments:
Post a Comment