Pienaar arejea kukipiga Afrika ya kusini
Nahodha wa zamani
wa timu ya taifa ya Afrika kusini Bafana bafana, Steven Pienaar,
amerejea nchini mwake na kujiunga na timu Bidwest Wits kwa mkataba wa
mwaka mmoja .
Pienaar mwenye umri wa miaka 35 amejiunga na timu
hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Sunderland ya nchini
England.Kiungo huyu amecheza soka la kulipwa barani ulaya kwa miaka 16 akicheza soka katika nchi za Uholanzi, Ujerumani na England,.
Baadhi ya vilabu alivyochezea mchezaji huyu ni Ajax, Everton, Borussia Dortmund, Tottenham Hotspur na Sunderland
No comments:
Post a Comment