Kampuni za simu zaingia matatani
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alitoa agizo hilo jana Dar es Salaam baada ya kukutana na wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi kutokana na kuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa huduma, zinazotolewa na kampuni hizo juu ya matangazo hayo, yanatolewa kabla ya mpigaji simu kuunganishwa.
Kilaba alisema hatua ya zuio la matangazo hayo kabla ya simu ya mteja kuunganishwa, linatokana na mamlaka hiyo kujiridhisha kuwa watoa huduma wengi wa mawasiliano ya simu za mkononi nchini, wamekuwa wakikiuka vigezo na masharti kama yanavyoelekezwa katika kanuni za huduma za ziada.
Hivyo, mamlaka imezuia kampuni hizo kusitisha mara moja utoaji wa matangazo hayo kuanzia jana Julai 6, 2017 ili kuondoa kero. Mtoa huduma yeyote ambaye atakiuka agizo hilo, atakabiliwa na adhabu kadhaa ikiwemo kufutiwa leseni ya kuendesha biashara ya utoaji wa huduma za mawasiliano nchini.
No comments:
Post a Comment