Friday, July 7, 2017

Teknolojia mpya ya uchenjuaji

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ndaki ya Uhandisi, wamekuja na teknolojia ya kuchenjua dhahabu kutoka kwenye mchanga kwa ajili ya wachimbaji wadogo wanaotumia zebaki ambayo ni hatari kwa afya zao.
Mhandisi migodi katika ndaki hiyo ya uhandisi chuoni hapo, Peter Kaheshi alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo katika Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kuhusu teknolojia hiyo. Kaheshi alisema katika mashine hiyo waliyoitengeneza, kemikali waliyoiweka haina athari kwa binadamu.

No comments:

Post a Comment