Man Utd wakubali kumnunua Romelu Lukaku kwa £75m
Manchester United wameafikiana na klabu ya Everton kulipa £75m kumchukua mshambuliaji Romelu Lukaku.
Raia huyo wa Ubelgiji wa miaka 24 alifunga mabao 26 katika Ligi ya Premia msimu uliopita.United, wamekuwa wakimtafuta Lukaku kwa kipindi kirefu majira haya ya joto.
Baada ya kumpata mshambuliaji huyo, sasa hawana haja tena ya kumtafuta Alvaro Morata wa Real Madrid.
Mazungumzo kuhusu kuhama kwa Lukaku hayahusiani na mazungumzo kuhusu uwezekano wa mshambuliaji wa United Wayne Rooney kurejea Everton.
- Lukaku kuondoka Everton msimu ujao
- Koeman: Lukaku ataondoka ili atimize ndoto yake
- Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 02.07.2017
Mshambuliaji huyo alikuwa miongoni mwa orodha ya wachezaji ambao Mourinho aliwasilisha kwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kwamba alitaka kuwanunua kabla ya msimu kumalizika.
Awali, ilidhaniwa Lukaku angerejea katika kalbu yake ya awali Chelsea, ambayo alijiunga nayo kutoka Anderlecht mwaka 2011.
Mshambuliaji huyo aliuziwa Everton kwa £28m na Mourinho mkufunzi huyo kutoka Ureno alipokuwa katika kipindi chake cha ukufunzi Chelsea mwaka 2014.
Lukaku ni mteja wa wakala Mino Raiola, ambaye pia huwasimamia Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan - wachezaji watatu walionunuliwa na United majira ya joto msimu uliopita.
Mbelgiji huyo alikataa ofa ya juu sana kutoka Everton Machi na kusema: "Sitaki kusalia katika kiwango sawa. Ninataka kujiboresha na najua ni wapi nahitaji kwenda kutimiza hilo."
Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 06.07.2017 na Salim Kikeke
Manchester United
wamewapiku Chelsea na kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku,
24, kwa kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni
75 (Daily Mail).
Manchester United wametoa dau la pauni milioni 66
kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, na
huenda makubaliano kati ya timu hizo mbili yakafikiwa katika saa chache
zijazo (Marca).Manchester United wangependa kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund Julian Weigl baada ya kushindwa kuwapata Eric Dier kutoka Tottenham na Nemanja Matic kutoka Chelsea (Daily Mail).
Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25 (Le10 Sport).
Atletico Madrid wanajiandaa kutoa dau rasmi la pauni milioni 22 kutaka kumsajili Diego Costa, 28, kutoka Chelsea (Guardian).
Chelsea wamefikia makubaliano na Roma ya kumsajili beki Antonio Rudiger, 24 kwa pauni milioni 34, ingawa mchezaji huyo bado hajafikia makubaliano rasmi kuhusu maslahi binafsi (Sky Sports).
Meneja wa zamani wa Liverpool Gerard Houllier anasema Arsenal huenda wamempata 'Ian Wright mpya' baada ya kumsajili Alexandre Lacazette (TalkSport).
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, ambao ni ongezeko la pauni 125,000 kwa wiki katika mshahara wake wa sasa (Daily Mirror).
Arsenal wametoa dau jipya kwa Monaco kutaka kumsajili winga Thomas Lemar (Evening Standard).
West Ham wanaonekana kuongoza katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, kwa pauni milioni 15 (Evening Standard).
Huddersfiled waliopanda daraja EPL wanakaribia kumsajili beki Mathias Jorgensen, 27, kutoka FC Copenhagen kwa pauni milioni 3.5 (Sun).
Kiungo wa Chelsea Nathaniel Chalobah, 22, anazungumza na Watford kutaka kuhamia katika timu hiyo aliyoichezea kwa mkopo msimu wa 2012-13 (Daily Mirror).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.
No comments:
Post a Comment