Kivumbi Yanga, Simba Okt 14
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema hayo jana Dar es Salaam. Alisema kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, kutakuwa na mechi ya Ngao ya Jamii kati ya timu hizo Agosti 23 Uwanja wa Taifa pia.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu, Simba ambao walimaliza wa pili katika ligi msimu uliopita itafungua dimba Agosti 26 na Ruvu Shooting. Mechi nyingine siku hiyo itakuwa kati ya Ndanda FC watakaowakaribisha Azam FC uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Siku hiyo pia Mwadui FC ya Shinyanga watawaalika Singida United na Mtibwa Sugar watacheza na Stand United Manungu. Kagera Sugar watawakaribisha Mbao FC ya Mwanza, Njombe Mji watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya na Mbeya City wataenda kuivaa Majimaji ya Songea, Ruvuma
.
Agosti 27 mabingwa watetezi Yanga, watashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Lipuli kutoka Iringa katika mchezo pekee siku hiyo. Lucas alizitaka klabu 16 zinazoshiriki ligi hiyo kukamilisha usajili wa Mtandao TMS kwa wakati kwani hawataongeza muda safari hii. Lucas alisema, Ligi inatarajiwa kumalizika Mei 20, 2018 na watajitahidi kusimamia ratiba yao isibadilike mara kwa mara ili kwenda na wakati.
No comments:
Post a Comment