Friday, July 7, 2017

Wakumbusha ahadi ya gari la wagonjwa

WAKAZI wa Muheza mjini wilayani hapa wamemuomba mbunge wa jimbo hilo, Adadi Rajabu kufuatilia ahadi ya kuleta gari la wagonjwa wilayani Muheza aliyoiacha rais mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofanya ziara yake ya mwisho mkoani Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema katika ziara yake ya mwisho Kikwete alikutana na wazee wa Muheza ambapo katika mazungumzo yao walimuomba kabla ya kumaliza kipindi chake cha uongozi awahakikishie anawatekelezea ahadi zake alizozitoa katika kampeni za urais.
Pia wamemuomba Rais John Magufuli kuhakikisha wilaya ya Muheza inaondokana na tatizo la uhaba wa maji lililopo kwa muda mrefu kwa kutekeleza mradi wa kuchukua katika chanzo cha maji katika mto Zigi uliopo katika milima ya Usambara tarafa ya Amani ambao kwa muda mrefu umezungumzwa lakini hautekelezwi

No comments:

Post a Comment