Kaburu mgonjwa Keko
MAKAMU wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange maarufu Kaburu, jana alishindwa kufi ka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam kwa kuwa anaumwa mahabusu ya Keko.
Taarifa hiyo ilitolewa mahakamani na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru), Leonard Swai. Swai alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Kisutu, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo ilikuja kutajwa lakini mshitakiwa anaumwa.
Mbali na Kaburu, mshitakiwa mwingine ni Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva aliyekuwepo kortini. Kaburu na Aveva wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo ya kughushi na kutakatisha fedha.
Hakimu Nongwa aliutaka upande wa mashitaka kukamilisha upelelezi haraka kwa sababu washitakiwa wapo rumande. Aliiahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika
No comments:
Post a Comment