Thursday, July 6, 2017

Malinzi wa BMT ‘out’


SERIKALI imeagiza kuvunjwa kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ikiwa ni mwendelezo wa kusafi - sha uozo katika sekta ya michezo nchini
.
Agizo hilo lilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jana mjini Dodoma wakati akiahirisha mkutano wa saba wa Bunge la Bajeti 2017/18. Alimwagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kulivunja
.
Alisema hawatafumbia macho usimamizi mbovu wa michezo usiojali maslahi ya Taifa. “Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo.

Haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa,” alisema. Hatua hiyo inamaanisha kuvunjwa kwa uongozi wa BMT chini ya Mwenyekiti, Dioniz Malinzi, kaka wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi aliyeko mahabusu akikabiliwa na kesi akidaiwa kutakatisha mamilioni ya fedha
.
Majaliwa alimwagiza Waziri Mwakyembe kufanya mapitio na tathmini ya uwepo wa BMT kujiridhisha kama inafaa iwepo au ivunjwe. “Namuagiza Waziri wa Michezo kulipitia Baraza la Michezo kujiridhisha na usimamizi wake wa michezo.

Naelekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) livunjwe, shughuli zake zitafanywa na sekretarieti hadi baraza jipya litakapoundwa,” alisema. Alimpongeza Rais John Magufuli kwa kuunga mkono uendelezaji michezo kwa kujenga uwanja wa kisasa wa kimataifa mjini Dodoma kwa msaada wa nchi rafiki ya Morocco.

Alilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwaendeleza na kuwatunza wachezaji wa timu ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ waliocheza fainali za vijana Afrika Gabon.
Aliipongeza Serengeti Boys kwa kuonesha upinzani mkubwa katika mashindano ya soka ya vijana wa chini ya miaka 17 AFCON akisema kwa upande wake timu hiyo ni washindi. “Binafsi nilifuatilia mechi zote za Serengeti Boys
 .
Nikiri kwamba vijana hao wana vipaji na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao. Kwangu mimi vijana wale ni washindi bila hata kuwapa taji lolote, kwani kanuni za mashindano ndizo zilizowafanya watolewe,” alisema Majaliwa.

Serengeti Boys iliondolewa ikiwa na pointi 4 sawa na Niger lakini ikazidiwa kwa tofauti ya mabao iliyofungwa (1-0) zilipokutana na Niger. “Msisitizo wangu kwa TFF ni kuendelea kuwatunza vijana hao na kusimamia klabu za michezo na kuwekeza kwenye soka la vijana ili tujenge timu imara kwa miaka ijayo,” alisema.

No comments:

Post a Comment