Friday, July 7, 2017

  CAF yavitupa nje vilabu vya Sudan Klabu Bingwa na Shirikisho


Kufuatia nchi ya Sudan kutimuliwa na FIFA baada ya serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka, Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), limeondoa vilabu vya soka vya nchi hiyo vilivyokuwa vinashiriki michuano mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

Vilabu vilivyotimuliwa ni pamoja na Al Merreikh iliyokuwa nafasi ya pili kundi A klabu Bingwa Afrika ikiwa na pointi saba ikiongozwa na Etoile du Sahel ya Tunisia. Timu nyingine ni Al Hilal Omdurman iliyo katika nafasi ya mwisho kundi A Klabu Bingwa Afrika ikiwa na pointi nne.
Timu nyingine ni Hilal El Obied Club iliyokuwa ikiongoza kundi C ikiwa na pointi 10 katika kombe la Shirikisho.

No comments:

Post a Comment