Dirisha la usajili linaendelea tu huku nchini Uingereza Manchester City wanaonekana kutembeza pesa sokoni na kuchukua yoyote wanayemtaka ili kuimalisha kikosi chao.
Manchester United hadi hivi sasa wamesajili wachezaji wawili tu lakini tetesi kuhusu usajili wao zimekuwa ni nyingi sana kuliko usajili wenyewe jinsi unavyokwenda.
Baada ya kumnunua Lindelof na Romelu Lukaku kulikuwa na taarifa kwamba Nemanja Matic na Ivan Perisic wako njiani kuelekea Old Traford na wakati wowote dili hizo zinaweza kukamilika.
Jose Mourinho alithibitisha kwamba United wanahitaji wachezaji wawili wengine haswa winga na kiungo mkabaji lakini hadi hivi sasa hakuna kinachoendelea.
Taarifa zinasema United wameshindwana na Inter kuhusu Perisic baada ya United kugoma kutoa £48m na pia hawataki kutoa £40m kwa Nemanja Matic na usajili wa Eric Dier nao unaonekana umeota mbawa.
Jose Mourinho amekosa furaha kutokana na hali ya usajili ndani ya klabu hiyo inavyoendelea na anaona familia ya Glazer na mkurugenzi Ed Woodward wanachukulia poa suala la kuleta wachezaji wapya.
Mourinho anakosa raha kwani hadi hivi sasa usjili aliopendekeza umekamilika kwa 50% tu huku 50% zilizobaki zinaonekana kama zimeota mbawa, hii leo United watakuwa uwanjani katika mchezo wa kirafiki zidi ya Vaaleranga ya nchini Norway.
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 28.07.2017 na Salim Kikeke
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionArsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sun)
Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sun)
Monaco wamekataa dau la tatu la Arsenal la pauni milioni 44.7 la kumtaka Thomas Lemar. (L'Equipe)
Image captionMeneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu, huku Manchester United wakimfuatilia. (Mirror)
Monaco watakuwa tayari kumuuza Kylian Mbappe kwa timu itakayokuwa tayari kutoa euro milioni 180. (L'Equipe)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutoa pauni milioni 50 kuwasajili Ross Barkley, 23, kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kutoka Arsenal. (Sun)
Chelsea wamepanda dau kutaka kumsajili kwa mkopo Renato Sanches, 19, kutoka Bayern Munich. (Daily Telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochetitino anataka kumsajili Ross Barkley na kumfanya kuwa kiungo wa kati. (Times)
Image captionRoma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)
Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)
Liverpool wapo tayari kutoa dau la mwisho la zaidi ya pauni milioni 70 kujaribu kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Mirror)
Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionLiverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)
Limerpool- kwa shingo upande- wameweka bei ya Philippe Coutinho kuwa ni pauni milioni 133, kama kweli Barcelona wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil. (Sport)
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema anataka Ivan Perisic kubakia Italia, ingawa hana uhakika kama ataweza kufanya hivyo huku Manchester United wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)
Image captionInter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)
Inter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)
Juventus wanaotafuta kiungo mkabaji sasa wamemgeukia Blaise Matuidi, 30, wa PSG, baada ya kuacha kumfuatilia Nemanja Matic, 28, anayenyatiwa na Manchester United. (Independent)
Mwenyekiti wa AC Milan Marco Fassone amesema klabu yake imezungumza na wakala wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28. (Sky Sports)
Image captionMshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)
Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala, 23, anayenyatiwa na Manchester United na Barcelona, hana mipango ya kuondoka Juventus msimu huu. (TalkSport)
Wakala wa mchezaji wa Arsenal Lucas Perez amekwenda London kuzungumzia kurejea kwa mshambuliaji huyo Deoportivo La Coruna. (AS)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfersTetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumaa Kareem.
Tiketi za kuuona mpambano kati ya Mayweather na McGregor $150000
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionNaymar kujiunga na PSG
Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki ijayo. (RMC)
PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil. (AS)
Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham kuziba pengo. (Mirror)
Image captionPhillip Coutinho
Barcelona wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool huenda ikawakatisha tamaa. (AS)
Kiungo wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 zina manufaa yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca)
Monaco wanasisitiza kuwa hawatamuuza Thomas Lemar, 21, licha ya Arsenal kupanda dau la tatu la takriban pauni milioni 45 kumtaka kiungo huyo. (Telegraph)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionManchester City wanasema kuwa watampatia Sanchez mshahara wa pauni 320,000 kwa wiki
Manchester City watampa Alexis Sanchez, 28, mshahara wa pauni 320,000 kwa wiki akijiunga nao kutoka Arsenal. (Mail)
Kipa wa Manchester City Claudio Bravo amesema Alexis Sanchez atapokelewa kwa mikono miwili akiamua kwenda Etihad. Bravo na Sanchez wote wanachezea timu ya taifa ya Chile. (24 Horas)
Southampton wamedhamiria kutomuuza beki wao Virgil van Dijk, 26, na watamrejesha katika kikosi cha kwanza licha ya kuachwa katika kikosi kilichokwenda mazoezini Ufaransa wiki hii (Telegraph)
West Ham watakataa dau lolote la kumtaka kiungo mshambuliaji wake Manuel Lanzini, 24. (Evening Standard)
Image captionAlvaro Negredo
Swansea wanakabiliwa na ushindani kutoka Leeds United katika kumsajili Alvaro Negredo, 31, aliyecheza kwa mkopo Middlesbrough msimu uliopita. (Mirror)
Manchester United wamenza mazungumzo ya mkataba mpya na Ander Herera, 27, ili kuzuia Barcelona kumnyatia kiungo huyo. (Express)
Manchester United wamerejea tena katika kumfuatilia winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28, lakini wana wasiwasi huenda wakamkosa kwa kuwa wamepoteza muda mwingi kumfuatilia Gareth Bale, 28, wa Real Madrid. (Independent)
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti anadhani mkataba wa Ivan Perisic kwenda Old Trafford haupo tena kutokana na kusuasua kwa mazungumzo kati ya Man Utd na Inter hivi karibuni. (Premium Sport)
Haki miliki ya pichaBBC SPORTImage captionGareth Bale atakataa hatua ya Real Madrid kumuuza kwenda Manchester United kwa sababu hana mpango wa kuondoka Madrid. (Times)
Gareth Bale atakataa hatua ya Real Madrid kumuuza kwenda Manchester United kwa sababu hana mpango wa kuondoka Madrid. (Times)
Mchezaji kinda kutoka Brazil, Gabriel Martinelli, 16, anafanya majaribio na Manchester United akitarajia kukamilisha uhamisho wake kutoka Ituano. (Manchester Evening News)
Liverpool wameacha kumfuatilia kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, na huenda wakarejea tena msimu ujao ambapo inaaminika huenda wakaweza kumsajili kwa pauni milioni 48. (Liverpool Echo)
Image captionRafinha
Liverpool, Arsenal na Tottenham, zote zinamnyatia kiungo wa Barcelona Rafinha msimu huu. (Mundo Deportivo)
Arsenal wanataka kumsajili kiungo Jakub Jankto, 21, kutoka Udinese. (SportItalia)
Chelsea watalazimika kutoa takriban pauni milioni 17.9 kama wanataka kumsajili kiungo wa Inter Milan Antonio Candreva. (Daily Star)
Everton watataka kumsajili kiungo wa Nice, Jean Seri, 26, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, ikiwa watashindwa kumpata Gylfi Sigurdsson, 27, kutoka Swansea. (L'Equipe)