Thursday, August 31, 2017
Uamuzi wa Msuva baada ya kukutwa na hatia ya kusukuma mwamuzi
ShaffihDauda / Dick Dauda / 16 minutes ago
Kamati ya nidhamu ya TFF leo August 31, 2017 imetangaza kumuandikia barua ya onyo kali Simon Msuva winger wa Taifa Stars na klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco kufuatia kukutwa na hatia ya kumsukuma mwamuzi kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita kati ya Mbao FC dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Wachezaji wengine waliohusishwa kwenye kesi kesi hiyo ni Obrey Chirwa na Deus Kaseke ambapo wawili hao hawajakutwa na hatia kwenye kesi hiyo.
“Maamuzi waliyotoa nayapokea kwa sababu hata kwa wachezaji wengine itawafundisha kwamba, maamuzi anayotoa refa ndio hayohayo ameamua kutoa. Naomba radhi kwa kilichotokea kwa sababu hakikutokea kwa pekeangu, tulikuwa wachezaji watatu mimi, Chirwa na Kaseke, mimi naomba radhi na wao najua wataomba radhi kwa muda wao,” Msuva.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment