Friday, August 11, 2017

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND JAPO KWA MBINDE, YASHINDA 4-3

Danny Welbeck akiwa amempanda mgongoni mshambuliaji mpya wa Arsenal, Alexandre Lacazette kutoka Lyon ya Ufaransa baada ya kuifungia The Gunners bao la kwanza dakika ya pili katika ushindi wa 4-3 kwenye mchezo wwa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England usiku wa Ijumaa Uwanja wa Emirates, London. Mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Welbeck dakika ya 45, Aaron Ramsey dakika ya 83 na Olivier Giroud dakika ya 85 wakati ya Leicester yamefungwa na Shinji Okazaki dakika ya tano, Marc Albrighton dakika ya 29 na Jamie Vardy dakika ya 56 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

No comments:

Post a Comment