Friday, October 20, 2017

MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2017/2018 YATANGAZWA SOMA ZAIDI.....

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS



MBARAKA, SURE BOY "BAMPA TO BAMPA" TUZO YA MWEZI AZAM FC

MABARA

Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji, Mbaraka Yusuph wameingia katika vita ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba ambayo hutolewa kila mwezi klabuni hapo.

Majina hayo ya wachezaji wa Azam yamependekezwa na viongozi wa timu hiyo akiwemo kipa wa kigeni Razark Abalola raia wa Ghana miongoni mwa wachezaji watatu walioingia katika kinyang’anyiro hicho. 

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffari Idd alisema kuwa, jopo la viongozi wamepitisha majina hayo ambayo yatapigiwa kura kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji na nidhamu kwa jumla.

“Kama ulivyo utaratibu wa Azam FC, jopo la viongozi wamepitisha majina matatu ya wachezaji akiwemo Sure Boy, Mbaraka na kipa Razark kwa ajili ya kuchuana katika tuzo ya Septemba ambapo mashabiki wa soka ndiyo watakaopata nafasi ya kupiga kura kupitia mitandao ya kijamii na atakayepata kura nyingi ndiyo atakayeibuka mshindi.

“Vigezo vitakavyozingatiwa ni nidhamu ya mchezaji, uwezo wa kujituma uwanjani na vitu vingine, vitu vyote hivyo vitaamuliwa na mashabiki kama ilivyo mwezi uliopita tulipompata mchezaji bora wa mwezi wa nane ambaye alikuwa Yakub Mohamed, hivyo tunawaomba wadau kufuatilia mechi zetu za Azam kisha kupiga kura na si kubuni,” alisema Jaffari.

Aidha, wachezaji hao walipoulizwa kuhusiana na tuzo hiyo walieleza kuwa, wamefurahishwa na hatua hiyo iliyochukuliwa na viongozi wao huku kila mmoja akiahidi kuitwaa tuzo hiyo na kudai kuwa itawaongezea morali ya kujituma zaidi katika kila mechi. 

Thursday, October 19, 2017

KUKOSEKANA KWA KAMUSOKO; ALICHOSEMA LWANDAMINA HIKI HAPA...



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amefunguka kuwa hakuna pengo lolote ndani ya kikosi chake licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao ni majeruhi.

Kocha huyo amesema hayo wakati wachezaji hao Jumamosi iliyopita walishindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kilishuka dimbani kumenyana na Kagera Sugar ambao walishinda kwa mabao 2-1, kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Kamusoko yuko nje akisumbuliwa na kifundo cha mguu (enka) ambapo atazikosa mechi zote za timu hiyo Kanda ya Ziwa dhidi ya Kagera Sugar na Stand United, huku Ngoma akisumbuliwa na majeraha ya goti.

Lwandamina amesema kwake haoni shida ya kutokuwa na wachezaji hao kwenye kikosi hicho kutokana na uwepo wa wachezaji wengine ambao wanaifanya kazi vizuri na kupata matokeo.

“Huwezi kusema kwamba kuna pengo la Ngoma au Kamusoko kwa sababu unapozungumzia timu ni juu ya watu wote ambao wapo na hali ya umoja iliyopo na siyo suala la mchezaji mmoja pekee, ndiyo maana utaona hatukuwa nao lakini tumepata matokeo mazuri.

“Kwangu hakuna pengo la mchezaji yeyote yule kutokana na waliopo kuifanya kazi vizuri na matokeo tunapata, kuna zaidi ya wachezaji 20 hapa sasa wanapokosekana wachezaji wawili au watatu hilo siyo pigo hata kidogo kwetu, kwani ninachukua mbadala wake na ninamtumia,” alisema kocha huyo wa zamani wa Zesco United ya Zambia.

SOURCE: CHAMPIONI

Thursday, September 21, 2017

Bomoabomoa jangwani

BOMOABOMOA JANGWANI: Kinachoendelea baada ya wananchi kuondolewa millardayo.com / Edwin Kamugisha TZA / 11 hours ago Jana wananchi waliokuwa wakiishi kwenye Bonde la Jangwani Dar es salaam waliondolewa na jiji kutokana na kuishi eneo hilo kinyume cha utaratibu. Haikuwa rahisi kwa bomoabomoa kutekelezwa eneo hilo baada ya wananchi kupambana na jeshi la polisi kuzuia bomoabomoa ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Jiji katika eneo hilo. Sasa leo AyoTV na millardayo.com zimefika eneo hilo […]

Simba wakwama kwa mbao waiacha mtibwa ijitawale

SIMBA WAKWAMA KWA MBAO, WAIACHA MTIBWA IJITAWALE SPORTS IN BONGO / 10 hours ago Mabingwa wa kombe la shirikisho Simba SC wamekwama kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kwenda sare ya goli 2-2 na Mbao FC mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba hiii leo. Simba SC waliuwanza mchezo wa leo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kuongoza kupitia kwa Shiza Kichuya katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Erasto Nyoni na kupelekea kipindi cha kwanza kumalizika kwa simba sc kuwa mbele kwa goli 1-0. Katika kipindi cha kwanza kulifanyika mabadiliko mawili ambapo Mbao FC walikuwa wa mwanzo kwa kumpumzisha Hebert Lukindo na kuingia Said Said katika dakika ya 39, huku Simba SC wakimtoa Shiza Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niypnzima katika dakika ya 45. Katika dakika ya 46 Mbao FC walisawazisha goli kupitia kwa Habibu Haji kabla James Kotea kuifungia Simba SC goli la pili katika dakika ya 48 akiunga mpira wa faulo uliopigwa na Erasto Nyoni. Mbao FC walisawazisha goli hilo katika dakika ya 83 kupitia kwa Boniface Maganga na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2. Matokeo ya mchezo huo inaifanya Simba SC kufikisha pointi 8 katika michezo 4 waliyoicheza wakiwa nyuma kwa pointi moja kwa vinara Mtibwa wenye pointi 9 katika michezo mitatu huku Azam FC akiwa nyuma ya Simba SC wakiwa na pointi 7 katika muchezo 3. 

Wednesday, September 20, 2017

BREAKING: Polisi wamemkamata Zitto Kabwe Airport DSM millardayo.com / Millard Ayo / 45 minutes ago

Jioni ya leo September 20 2017 imetoka taarifa kwamba Mbunge wa Kigoma Mjini ambae pia ni kiongozi wa Chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi. Taarifa hizo zimethibitishwa na ACT WAZALENDO ambao wamesema ni kweli Zitto amekamatwa akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam akitokea Kigoma, kwa sasa Wanasheria wa chama wanafatilia kujua […]

Saturday, September 9, 2017

Umati wa watu wakiwa Katika Mtaa wa olkereian Kata ya Olasiti Ambapo watoto wawili Morin na Ikram ambao walitekwa mkoani Arusha

Umati wa watu wakiwa Katika Mtaa wa olkereian Kata ya Olasiti Ambapo watoto wawili Morin na Ikram ambao walitekwa mkoani Arusha wamepatikana wakiwa wametumbukizwa katika kisima cha maji wakati askari wakiwa wanafanya jitihada za kupasua kisima ambacho watoto waliotekwa wametumbukizwa humo Hataivyo askari waliofika katika eneo hilo wamefanikiwa kutoa miili ya watoto hao wawili na kufikisha katika eneo husika kwa uchunguzi zaidi.........Usiache kufuatilia Ukurasa huu kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili. Image may contain: 1 person, crowd and outdoor

Umati wa watu wakiwa Katika Mtaa wa olkereian Kata ya Olasiti Ambapo watoto wawili Morin na Ikram ambao walitekwa mkoani Arusha wamepatikana wakiwa wametumbukizwa katika kisima cha maji wakati askari wakiwa wanafanya jitihada za kupasua kisima ambacho watoto waliotekwa wametumbukizwa humo
Hataivyo askari waliofika katika eneo hilo wamefanikiwa kutoa miili ya watoto hao wawili na kufikisha katika eneo husika kwa uchunguzi zaidi.........Usiache kufuatilia Ukurasa huu kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili.

Tuesday, September 5, 2017

Umati wa watu wakiwa Katika Mtaa wa olkereian Kata ya Olasiti Ambapo watoto wawili Morin na Ikram ambao walitekwa mkoani Arusha wamepatikana wakiwa wametumbukizwa katika kisima cha maji wakati askari wakiwa wanafanya jitihada za kupasua kisima ambacho watoto waliotekwa wametumbukizwa humo Hataivyo askari waliofika katika eneo hilo wamefanikiwa kutoa miili ya watoto hao wawili na kufikisha katika eneo husika kwa uchunguzi zaidi.........Usiache kufuatilia Ukurasa huu kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili. Image may contain: 1 person, crowd and outdoor

Umati wa watu wakiwa Katika Mtaa wa olkereian Kata ya Olasiti Ambapo watoto wawili Morin na Ikram ambao walitekwa mkoani Arusha wamepatikana wakiwa wametumbukizwa katika kisima cha maji wakati askari wakiwa wanafanya jitihada za kupasua kisima ambacho watoto waliotekwa wametumbukizwa humo
Hataivyo askari waliofika katika eneo hilo wamefanikiwa kutoa miili ya watoto hao wawili na kufikisha katika eneo husika kwa uchunguzi zaidi.........Usiache kufuatilia Ukurasa huu kwa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hili.

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

post-feature-image

Kijana wa Miaka 18 Asimulia Jinsi Alivyowateka Watoto Wanne Arusha

Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alip...
 Afariki Kanisani Baada ya Kutoa Sadaka
 Makubwa Haya: MWIZI AKUTWA AMELALA FOFOFO KITANDANI KWENYE NYUMBA ALIYOVUNJA
 TANZIA... BILIONEA MAARUFU JIJINI ARUSHA NA MILIKI WA IMPALA, NAURA NA NGURDOTO HOTEL AFARIKI DUNIA

Matukio ya utekaji watoto mjini Arusha yameanza kupata mwelekeo wa ufumbuzi baada ya kijana wa miaka 18 kukiri kuwateka watoto wanne alipokamatwa katika mji wa Katoro wilayani Geita alikofanya tukio jingine la utekaji. 


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari akiwa chini ya ulinzi wa polisi jana, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Samson Petro alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000. 


Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fedha walichotakiwa kumpa. 


Samson alisema alianza ‘shughuli’ hiyo ya utekaji watoto kutokana na mahitaji ya fedha na kwamba, aliacha shule akiwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Lutozo iliyopo Katoro. 


“Naishi na wazazi wangu, lakini nao ni masikini, nilifanya hivi ili nipate fedha na nilikuwa nikimchukua mtoto naandika ujumbe kwenye karatasi, naandika na namba ya simu napeleka karibu na familia ili wanitafute,” alisema Samson. 


Awali, kamanda wa polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema walimkamata kijana huyo katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mjini Katoro juzi saa mbili usiku. 

Mwabulambo alisema polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha walifanya uchunguzi na kubaini mtuhumiwa alikuwa Katoro. 


Alisema walipata taarifa za kutekwa Justin Ombeni (2) Septemba Mosi nyumbani kwao katika eneo la Shilabela ambako mtuhumiwa alikwenda na kuwakuta watoto wanne wakicheza nyuma ya nyumba. 


Alisema aliwagawia pipi na kuondoka na Justin. Kamanda huyo alisema polisi ilipata taarifa kuwa kijana huyo yupo chumba namba 103 katika nyumba hiyo ya wageni ambako waliweka ulinzi kuizunguka. 


Alisema walipoingia katika chumba hicho walimkuta akiwa na 
mtoto huyo. Mwabulambo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika. 


Ombeni Mshana ambaye ni baba wa Justin alisema mtekaji huyo alimpatia ujumbe mtoto wa jirani uliomtaka kutuma Sh4 milioni na walipokuwa wakiwasiliana na mtuhumiwa alishusha kiwango hadi Sh1 milioni. 


Alisema polisi walimtahadharisha kwamba asitume fedha hizo.Kamanda Mwabulambo alisema tukio la kutekwa Justin ni la pili katika kipindi cha miezi minne baada ya mwingine kutekwa. 

Kesi kuhusu tukio hilo la kwanza inaendelea mahakamani baada ya mtoto kupatikana. 

Katika hatua nyingine, kikosi kilichoundwa na wananchi mkoani Arusha kikiongozwa na mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Kata ya Olasiti, Daudi Safari na familia za watoto wawili waliotekwa kimewakamata watuhumiwa wawili na kuwafikisha polisi. 


Watoto hao ambao bado hawajapatikana ni Moureen David (6) anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Lucky Vincent na Ikram Salim (3). 


Wakizungumza jana nje ya kituo kikuu cha polisi Arusha baada ya kuwafikisha kituoni watuhumiwa hao, Safari na wazazi wa watoto hao, David Njau na Salim Kassim walisema kwa nyakati tofauti wameanzisha msako baada ya 
kuona siku zinakwenda bila watoto kupatikana. 


Moureen alitekwa Agosti 21 saa 11 jioni akiwa anacheza nyumbani kwao eneo la Olasiti, wakati Ikram alitekwa Agosti 26 saa 12 jioni akiwa anacheza na watoto wenzake nyumbani kwao, Burka - Olasiti. 


Safari alisema wamemkamata mtu mmoja (jina linahifadhiwa) 
ambaye simu yake ilitumiwa na watekaji kuomba fedha kwa mzazi wa Ikram Salim. 


Alisema pia wamemkamata wakala wa fedha wa kampuni moja ya simu (jina tunaihifadhi) aliyetoa Sh300,000 kwa watekaji baada ya fedha kutumwa na mzazi wa Ikram. 


Imeelezwa kuwa wakala huyo amekamatwa kwa kuwa fedha hizo zilitolewa pasipo kuorodheshwa popote na mpokeaji hakuonyesha kitambulisho chochote. 


Akizungumzia operesheni hiyo, Njau alisema hawatapumzika mpaka watoto wao wapatikane. 

Alisema ufuatiliaji walioufanya kupitia minara ya kampuni za simu unaonyesha wahusika walikuwa eneo la Kwa Mrombo jijini Arusha walipopiga kuomba Sh4.5 milioni ili wamwachie Doreen na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya Ikram. 


Watekaji hao kupitia ujumbe waliotuma nyumbani kwa Njau walidai kama wasipopewa fedha wangempoteza mtoto huyo japokuwa hawana nia hiyo. 

Kassim Salim ambaye ni babu wa Ikram alisema, “tunaendelea kuomba msaada zaidi kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na vyombo vya dola watusaidie tuwapate watoto wetu.” 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema juzi kuwa watu watatu wanashikiliwa wakihusishwa na tukio hilo akiwapo dereva wa bodaboda mkazi wa Olasiti aliyetumwa kuwarejesha watoto wawili waliokuwa wametekwa. 


Matukio ya utekaji yalianza kuibuka Agosti 21 baada ya kutekwa watoto wanne. Watoto wawili Ayoub Fred na Bakati Selemani wakazi wa eneo la FFU, kata ya Murieti jirani na kata ya Olasiti walirejeshwa

Mifuko ya jamii yageukia uchumi wa viwanda EAC

Mifuko ya jamii yageukia uchumi wa viwanda EAC

KATIKA kuitikia wito wa Serikali ya Rais John Magufuli wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda, Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), unakusudia kufufua viwanda 25 ambavyo vimeshindwa kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 baada ya Serikali kuvibinafsisha.
Hatua hiyo inalenga kusaidia kukuza uchumi wa nchi, lakini pia kuibua ajira zaidi, ikiwezekana asilimia 40 ya ajira katika sekta ya viwanda Tanzania itokane na uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii, huku bidhaa zake zikiwa za kiwango cha juu kwa ajili ya soko la ndani na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Katibu wa TSSA, Meshack Bandawe ambaye ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Bandawe amesema mbali ya kufufua viwanda hivyo, pia mifuko ya hifadhi za jamii inatarajiwa kujenga viwanda vipya katika sehemu mbalimbali za nchi ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Alitoa mfano kuwa mbali ya mfuko mmoja mmoja, kuna miradi ya pamoja ukiwamo wa Kiwanda cha Morogoro Canvas ambacho ni cha kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa utengenezaji wa nguo ngumu, zikiwemo sare za majeshi, shuka za hospitali, sare za wafungwa na maturubai.
Kiwanda hicho kitakapoanza tena uzalishaji wakati wowote kuanzia mwanzoni mwa mwaka ujao, kinatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 700. “Tumeiona hiyo fursa, hivyo lazima tuchangamkie kukifufua na kuzalisha bidhaa hizi kwa ajili ya soko la Afrika Mashariki,” alisema Bandawe.
Aliitaja mifuko inayoshiriki katika mradi huo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), PPF, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali Kuu (GEPF) na Shirika la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Umoja wa mifuko pia umeweka nguvu ya pamoja na kuelekeza katika kufufua vinu vya pamba, ikianza na vitatu ambavyo vinatarajiwa kuzalisha ajira za viwandani 1,200, lakini wakulima zaidi ya 7,000 wakitarajiwa kunufaika kutokana na umoja huo kulenga kufufua mashamba makubwa ya pamba.
Wanakusudia pia kuwekeza katika viwanda vya nguo vya Urafiki kilichopo Dar es Salaam na Mwatex cha Mwanza, achilia mbali katika sekta ya ngozi ambako wanatarajia kuwa na kiwanda kikubwa cha bidhaa za ngozi.
“Kwa ujumla tunataka kuitikia wito wa Rais wa kuwa na viwanda vitakavyoajiri wengi, vitakavyokuwa na mnyororo mrefu wa thamani kuanzia kilimo, malighafi na kadhalika kutoka hapahapa nchini, lakini bidhaa zikivuka mipaka.
Hii ina maana tutahakikisha pia vinakuwa na ubora wa kimataifa,” alisema na kuongeza kuwa, kwa kuanzia, ikianza kabla ya mwaka 2019, itatoa ajira zaidi ya 200,000. Akizungumzia viwanda 25, alisema 15 vimeshapata idhini ya kuendelezwa huku vingine 13 vikiwa katika hatua ya upembuzi yakinifu.
Alitoa mfano kuwa NSSF imewekeza katika kiwanda cha kuua viuatilifu vya malaria kilicho Kibaha mkoa wa Pwani, imefufua vinu vya kusindika nafaka vya Shirika la Taifa la Usagishaji (NMC) vya Iringa, Dodoma na Mwanza vitakavyotoa ajira 30,000, Kiwanda cha Matairi cha General Tyre mkoani Arusha, kinacholenga kutengeneza matairi ya kisasa kwa ajili ya soko la ndani nanje ya nchi.
NSSF itawekeza pia katika Kiwanda cha Chaki cha Maswa mkoani Simiyu, Kiwanda cha Sukari cha Lulanzi kitakachozalisha pia umeme. Inaelekeza pia nguvu katika kilimo cha katani na kuboresha uzalishaji za bidhaa za katani, huku ikishirikiana PPF na Magereza katika kilimo cha miwa na kufufua viwanda vya sukari vya Mkulazi na Mbigiri mkoani Morogoro.
Kwa upande wa PPF, mbali ya ubia na NSSF katika mashamba na viwanda vya Mkulazi na Mbigiri, pia inawekeza katika kiwanda cha viatu na bidhaa za ngozi kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza mkoani Kilimanjaro, huku ikiwa na mipango ya kujenga kiwanda cha kuchakata ngozi kinachotarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka kesho.
Nayo PSPF, pamoja na kufufua Kiwanda cha Dawa cha TPI cha Arusha, itajenga pia kiwanda cha matofali na kuchoma vigae Dodoma, kiwanda cha vifaa ya umeme na nguzo za zege, lakini pia soko la kisasa la kuuza mazao.
Kwa upande wa LAPF inakusudia kujenga machinjio ya kisasa ya Nguru, Mvomero mkoani Morogoro itakayokuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 300 kwa siku, lakini pia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa Kiwanda cha Tangawizi cha Same mkoani Kilimanjaro.
NHIF inawekeza katika ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za pamba kwa matumizi ya hospitali, kiwanda cha maji-tiba, vyote vikiwa mkoani Simiyu. WCF inawekeza kwa kushirikiana na GEPF katika kujenga viwanda vya juisi na mvinyo kutokana na zabibu, wakati ZSSF inajikita katika viwanda vya kisasa vya usindikaji wa samaki. GEPF itafufua pia kiwanda cha zana za viwandani cha Kilimanjaro

Wabunge Ukawa wagoma kuingia bungeni kuapishwa wabunge CUF


Wabunge Ukawa wagoma kuingia bungeni kuapishwa wabunge CUF

WABUNGE wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, leo wamegoma kuhudhuria kuapishwa kwa Wabunge wapya wa viti maalum kutoka Chama cha wananchi CUF, kazi iliyofanyika Bungeni na kuongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Wakiwa wamevalia nguo nyeusi wabunge hao kutoka vyama vyote vya upinzani bungeni hata wale wa CUF walikuwa katika makundi nje ya Ukumbi wa Bunge katika jengo la zamani la Ukumbi wa Pius Msekwa.
Baadae baada ya kukamilika uapishaji wa wabunge wapya ndani ya ukumbi wa Bunge, waliandamana kwa pamoja hadi katika lango kuu la Bunge na kukusanyika kasha kuzungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi wao huo wa kugomea shughuli ya kuapisha Wabunge wapya wa kambi hiyo Bungeni.
Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mbunge wa Momba, kupitia Chama cha Demorasia na Maendeleo Chadema, David Silinde alizungumza na wanahabari na kusema kuwa wamefanya hivyo kuunga mkono wenzao waliofukuzwa na kufungua kesi Mahakamani.
Silinde alisema hawatawaunga mkono wala kushirikiana na wabunge hao wapya wa CUF hadi Kesi ya Msingi iliyopo Mahakamani itakapo kamilika. “Tumefanya hivi na tutaendelea na msimamo wetu wa kutoshirikiana na wabunge hawa hadi pale kesi ya Msingi itakapoisha Mahakamani,” amesema Silinde.

Thursday, August 31, 2017

Uamuzi wa Msuva baada ya kukutwa na hatia ya kusukuma mwamuzi ShaffihDauda / Dick Dauda / 16 minutes ago Kamati ya nidhamu ya TFF leo August 31, 2017 imetangaza kumuandikia barua ya onyo kali Simon Msuva winger wa Taifa Stars na klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco kufuatia kukutwa na hatia ya kumsukuma mwamuzi kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita kati ya Mbao FC dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wachezaji wengine waliohusishwa kwenye kesi kesi hiyo ni Obrey Chirwa na Deus Kaseke ambapo wawili hao hawajakutwa na hatia kwenye kesi hiyo. “Maamuzi waliyotoa nayapokea kwa sababu hata kwa wachezaji wengine itawafundisha kwamba, maamuzi anayotoa refa ndio hayohayo ameamua kutoa. Naomba radhi kwa kilichotokea kwa sababu hakikutokea kwa pekeangu, tulikuwa wachezaji watatu mimi, Chirwa na Kaseke, mimi naomba radhi na wao najua wataomba radhi kwa muda wao,” Msuva. 

Monday, August 21, 2017

Daktari wa taifa stars ya maximo afariki dunia

DAKTARI WA TAIFA STARS YA MAXIMO AFARIKI DUNIA BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE / 1 hour ago Na Salum Vuai, ZANZIBAR ALIYEWAHI kuwa daktari mkuu wa timu ya soka ya Taifa Tanzania, Taifa Stars Abdallah Said Mohammed al-maaruf ‘Kuku’, amefariki dunia usiku wa jana Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alilitumikia benchi la ufundi Taifa Stars wakati kikosi hicho kikinolewa na Marcio Maximo kutoka Brazil na msaidizi wake Mzanzibari, Ali Bushiri, ambacho kilifanikiwa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2009 nchini Ivory Coast.  Jeneza lililobeba mwili wa marehemu (katika picha ndogo kushoto) likitolewa msikiti maiti, Michenzani baada ya kusaliwa kuelekea malazoni. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema Peponi. Amin. Aidha aliwahi kuwa daktari wa timu ya taifa ya vijana U-20 wakati huo ikiitwa Karume Boys. Marehemu amezikwa leo mchana kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, ambapo mazishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Zanzibar wakiwemo wanamichezo, madaktari na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali alizozifanyia kazi ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) akihudumu katika kiwanja cha kufurahisha watoto Kariakoo kilicho chini ya mfuko huo

Sunday, August 20, 2017

Hatimaye wanachama wa simba wapitisha mabadiliko,Mwanachama mmoja akataa

BREKING NEWS: HATIMAYE WANACHAMA WA SIMBA WAPITISHA MABADILIKO, MWANACHAMA MMOJA AKATAA SALEH 





Hatimaye kwa pamoja, wanachama wa klabu ya Simba, wamepitisha mabadiliko ya klabu yao huku mwanachama mmoja tu akikataa. Wanachama waliofanya mkutano kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, wamekubaliana sasa klabu hiyo imeingia katika mfumo wa endeshwiaji utakaohusishwa uuzaji wa hisa.

Walichopitisha wanachama wa 1,216 wa simba kwenda kwenye mabadiliko

WALICHOPITISHA WANACHAMA WA 1,216 WA SIMBA KWENDA KWENYE MABADILIKO,
 Wanachama 1,216 wa klabu ya Simba, leo wamepitisha uamuzi wa klabu yao kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa hisa. Mwanachama mmoja pekee katika mkutano huo, ndiye alionyesha hisia zake kwa kupinga mfumo huo. Wanachama bado wataendelea kubaki kuwa wamiliki wa klabu hiyo kwa asilimia 50 huku wawekezaji nao wakilimiliki kwa asilimia 50 pia. Mbadiliko yaliyopitishwa na wanachama wa Simba yako hivi, wanachama watamiliki klabu yao kwa 50% huku 50% zikilikiwa na wawekezaji. Wawekezaji au mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Sh bilioni 20 katika uwekezaji huo sawa na wanachama. Kwa wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao watatakiwa kuchangia Sh bilioni 4 tu ambazo nia silimia 10 huku 40 ambayo ni bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao. Suala la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati baada ya watu kujitokeza, nayo itaandaa mkutano kuwaita wanachama kuwaeleza waliojitokeza katika uwekezaji ni akina nani. Wawekezaji wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.

Thursday, August 17, 2017

Msichana wa miaka 10 aliyebakwa India ajifungua mtoto

Msichana wa miaka 10 aliyebakwa India ajifungua mtoto

A protest in India against child sex abuseHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaandamano ya kupinga dhuluma za kingono dhidi ya watoto India
Msichana wa umri wa miaka 10 ambaye alinyimwa ruhusa ya kuavya mimba na mahakama ya juu zaidi nchini India mwezi uliopita amejifungua mtoto msichana.
Msichana huyo hajafahamu kuwa amejifungua. Wakati akiwa na uja uzito aliambiwa kuwa tumbo lake kubwa lilitokana na jiwe kubwa lililokuwa ndani ya tumbo.
Mtoto huyo mwenye uzito wa kilo 2.5 alizaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Chandigarh.
Mama na mtoto wote wako hali nzuri, afisa mmoja aliiambia BBC.
Msichana huyo anadaiwa kubakwa mara kadha katika kipindi cha miezi saba iliyopita na mjomba wake ambaye wa sasa amekamatwa.
Mimba yake iligunduliwa karibu mwezi mmoja uliopita wakati alilalamikia maumivu ya tumbo na wazazi wake wakampeleka hospitalini.
Mwezi uliopita mahakama ya juu ilikataa kumruhusu kuavya mimba hiyo kwa misingi kuwa alikuwa mdogo sana kuwa mjamzito, baada ya madaktari kusema kuwa kuavya mimba hiyo ya wiki 32 yaweza kuhatarisha maisha yake.