Tuesday, March 12, 2019

Polisi wathibitisha kifo cha Emiliano Sala

Polisi Uingereza wamethibitisha kuwa mwili uliopatikana katika mabaki ya ndege iliyokutwa imezama baharini ni wa nyota wa Klabu ya Cardiff, Emiliano Sala.

 Nyota huyo na rubani wake walitoweka Januari 21, 2019 wakiwa njiani kurudi Uingereza, hata hivyo hadi sasa mwili wa rubani bado haujapatikana.

Ndege hiyo, Piper Malibu N264DB ilikuwa ikitoka Ufaransa kwenda Cardiff, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina kurudi kwa safari ya haraka katika klabu yake ya zamani Nantes siku mbili baada ya kutangazwa kuidhinishwa kwa mkataba wake wa thamani ya £15m kwenda Cardiff .

Saturday, February 10, 2018

Msigwa abanwa, atakiwa kuwasilisha vielelezo bungeni



Msigwa abanwa, atakiwa kuwasilisha vielelezo bungeni

Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amemwagiza Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) kuwasilisha nyaraka zinazodai kuwa na habari mbaya za rushwa katika Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu ya utengenezaji wa pasipoti za kielektroniki uliozinduliwa hivi karibuni.
Msigwa alidai bungeni jana kuwa, chama chake cha Chadema, kimepata nyaraka zinazoonesha gharama ya pasipoti za kielektroniki ambayo ilizinduliwa na Rais John Magufuli, hazikufuata taratibu za ununuzi wa haki.
Wakati wa uzinduzi wa pasipoti za kielektroniki, serikali ilibainisha kuwa hati hizo zitatolewa kwa gharama ya Sh 150,000 ambazo zitadumu kwa miaka 10. Mradi wa pasipoti za kielekroniki unatekelezwa na Ireland na Kampuni HID ya Marekani kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 57.82.
Hata hivyo, Msigwa alibua suala la mradi huo wakati wa kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika kipindi cha Januari 2017 hadi Januari 2018.
“Wakati mfumo huu unazinduliwa, hatukuambiwa ikiwa ni pasipoti za kielektroniki au uhamiaji. Umma unadhani unahitaji kuwambiwa kipi ni kipi. Tunahitaji ufafanuzi kwenye suala hili,” alisema.
Tuhuma hizo zilimfanya Naibu Spika, Dk Ackson kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kupeleka nyaraka kwenye Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge yenye uwezo wa kuchunguza na kutoa ushauri hatua gani zichukuliwe kuhusu jambo hilo.
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba alimtaka Msigwa kutopotosha umma kwani mfumo wa pasipoti za kielektroniki haulengi hati ya kusafiria pekee, bali pia unajumusha utoaji huo wa viza za kielektroniki (e-Visa), vibali vya ukaazi vya kielektroniki (e-Permit) na udhibiti wa mipaka wa kielektronikia.
Hivi karibuni, Idara ya Uhamiaji ilibainisha ufisadi wa Sh bilioni 400, zilizolengwa kuhujumiwa kupitia zabuni ya utengenezaji wa pasipoti mpya za kielektroniki za kusafiria. Pia lilibainisha hujuma mpya ya kuwepo kwa kundi la wanasiasa linalotumiwa kufanya siasa chafu za kudhoofisha mchakato wa utoaji hati mpya za kielektroniki za kusafiria na kuwataka kuacha kufikiria maslahi yao na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
Hivi karibuni, Rais Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria za kielektroniki, alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo, ambao walipanga kufisidi Sh bilioni 400, bila mafanikio

Friday, October 20, 2017

MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2017/2018 YATANGAZWA SOMA ZAIDI.....

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS



MBARAKA, SURE BOY "BAMPA TO BAMPA" TUZO YA MWEZI AZAM FC

MABARA

Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji, Mbaraka Yusuph wameingia katika vita ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba ambayo hutolewa kila mwezi klabuni hapo.

Majina hayo ya wachezaji wa Azam yamependekezwa na viongozi wa timu hiyo akiwemo kipa wa kigeni Razark Abalola raia wa Ghana miongoni mwa wachezaji watatu walioingia katika kinyang’anyiro hicho. 

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffari Idd alisema kuwa, jopo la viongozi wamepitisha majina hayo ambayo yatapigiwa kura kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji na nidhamu kwa jumla.

“Kama ulivyo utaratibu wa Azam FC, jopo la viongozi wamepitisha majina matatu ya wachezaji akiwemo Sure Boy, Mbaraka na kipa Razark kwa ajili ya kuchuana katika tuzo ya Septemba ambapo mashabiki wa soka ndiyo watakaopata nafasi ya kupiga kura kupitia mitandao ya kijamii na atakayepata kura nyingi ndiyo atakayeibuka mshindi.

“Vigezo vitakavyozingatiwa ni nidhamu ya mchezaji, uwezo wa kujituma uwanjani na vitu vingine, vitu vyote hivyo vitaamuliwa na mashabiki kama ilivyo mwezi uliopita tulipompata mchezaji bora wa mwezi wa nane ambaye alikuwa Yakub Mohamed, hivyo tunawaomba wadau kufuatilia mechi zetu za Azam kisha kupiga kura na si kubuni,” alisema Jaffari.

Aidha, wachezaji hao walipoulizwa kuhusiana na tuzo hiyo walieleza kuwa, wamefurahishwa na hatua hiyo iliyochukuliwa na viongozi wao huku kila mmoja akiahidi kuitwaa tuzo hiyo na kudai kuwa itawaongezea morali ya kujituma zaidi katika kila mechi. 

Thursday, October 19, 2017

KUKOSEKANA KWA KAMUSOKO; ALICHOSEMA LWANDAMINA HIKI HAPA...



Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amefunguka kuwa hakuna pengo lolote ndani ya kikosi chake licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma ambao ni majeruhi.

Kocha huyo amesema hayo wakati wachezaji hao Jumamosi iliyopita walishindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kilishuka dimbani kumenyana na Kagera Sugar ambao walishinda kwa mabao 2-1, kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Kamusoko yuko nje akisumbuliwa na kifundo cha mguu (enka) ambapo atazikosa mechi zote za timu hiyo Kanda ya Ziwa dhidi ya Kagera Sugar na Stand United, huku Ngoma akisumbuliwa na majeraha ya goti.

Lwandamina amesema kwake haoni shida ya kutokuwa na wachezaji hao kwenye kikosi hicho kutokana na uwepo wa wachezaji wengine ambao wanaifanya kazi vizuri na kupata matokeo.

“Huwezi kusema kwamba kuna pengo la Ngoma au Kamusoko kwa sababu unapozungumzia timu ni juu ya watu wote ambao wapo na hali ya umoja iliyopo na siyo suala la mchezaji mmoja pekee, ndiyo maana utaona hatukuwa nao lakini tumepata matokeo mazuri.

“Kwangu hakuna pengo la mchezaji yeyote yule kutokana na waliopo kuifanya kazi vizuri na matokeo tunapata, kuna zaidi ya wachezaji 20 hapa sasa wanapokosekana wachezaji wawili au watatu hilo siyo pigo hata kidogo kwetu, kwani ninachukua mbadala wake na ninamtumia,” alisema kocha huyo wa zamani wa Zesco United ya Zambia.

SOURCE: CHAMPIONI

Thursday, September 21, 2017

Bomoabomoa jangwani

BOMOABOMOA JANGWANI: Kinachoendelea baada ya wananchi kuondolewa millardayo.com / Edwin Kamugisha TZA / 11 hours ago Jana wananchi waliokuwa wakiishi kwenye Bonde la Jangwani Dar es salaam waliondolewa na jiji kutokana na kuishi eneo hilo kinyume cha utaratibu. Haikuwa rahisi kwa bomoabomoa kutekelezwa eneo hilo baada ya wananchi kupambana na jeshi la polisi kuzuia bomoabomoa ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Jiji katika eneo hilo. Sasa leo AyoTV na millardayo.com zimefika eneo hilo […]