Polisi Uingereza wamethibitisha kuwa mwili uliopatikana katika mabaki ya
ndege iliyokutwa imezama baharini ni wa nyota wa Klabu ya Cardiff,
Emiliano Sala.
Nyota huyo na rubani wake walitoweka Januari 21, 2019 wakiwa njiani
kurudi Uingereza, hata hivyo hadi sasa mwili wa rubani bado
haujapatikana.
Ndege hiyo, Piper Malibu N264DB ilikuwa ikitoka Ufaransa kwenda Cardiff,
baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina
kurudi kwa safari ya haraka katika klabu yake ya zamani Nantes siku
mbili baada ya kutangazwa kuidhinishwa kwa mkataba wake wa thamani ya
£15m kwenda Cardiff .